kenyatta
university
|
MWONGOZO WA TAMTHILIA YA KIFO KISIMANI BY
KITHAKA WA MBERIA
|
Compiled by Amos Sifuna Barasa
|
|
student
|
31/1/2019
|
|
BY AMOS SIFUNA BARASA,
KENYATTA UNIVERSITY
TAMTHILIA YA KIFO KISIMANI
UTANGULIZI
Tamthilia ya Kifo Kisimani imeandikwa
na kithaka wa Mberia. Toleo la kwanza la kitabu hiki ililikuwa mwaka wa 2001 na
kina chapa nyingi hadi kufikia mwaka wa 2009.kimechapishwa na Marimba
Publications Ltd.
Anwani
Anwani huwa ni jina la kitabu.Mwandishi amefaulu
kutumia anwani’Kifo Kisimani’. Anwani hii inaashiria kifo cha Mwelusi pale
kisimani alipouliwa na Gege.
Pia anwani hii inaashiria kifo cha Wanabutangi baada
ya kukosa maji pale kisimani.Hii ni baada ya kanuni mpya za utekaji
maji kutolewa amabazo ziliwanyima haki za kuteka maji. Maji ni uhai hivyo
kupewa siku tatu za kuteka maji ni kunyimwa uhai yaani kifo.
Jalada
Jalada ni karatasi ngumu inayofunika kitabu ambapo
jina la kitabu huandikwa.Katika tamthilia hii kuna picha ya mtu aliye na huzuni.Mtu huyu
ni kama ako katika shimo. Hii inaashiria shimo la mateso ambalo Wanabutangi
wametiwa na utawala mbaya wa Bokono na vibaraka wake.
Kuna picha inayoashiria machea.Hii inaonyesha
matumaini kwa Wanabutangi baada ya Mwelusi na wenzake kuanza harakati za mabadiliko.Rangi inayotumika
kwa picha ni ya udongo, kuashiria rotuba ya Butangi.
DHAMIRA YA MWANDISHI
Kiini cha jambo au habari iliyoandikwa na
mwandishi.Katika Kifo Kisimani Kithaka wa Mberia ananuia kuamsha au kumchangamsha
msomaji kuhusu utawala mbaya na jinsi ya kuleta mabadiliko na kuuondoa .
Mwandishi anatetea haki za walionyanyaswa.Hivyo lengo
kuu la mwandishi ni kuzindua watu.
PLOTI
Huwa ni mtiririko wa matukio katika kitabu.Tamthilia
hii ina onyesho kumi.Muhtasari wa onyesho hizi ni kama ifuatavyo.
Onyesho la kwanza
Mchezo unaanza asubuhi ambapo viti vimepangwa tayari
kwa mkutano wa Bokono.Mwelusi ambaye ni kijan anaingia uwanjani.Mawazo yake
yanadhihirika kupitia kwa sauti tunayosikia .Yanamkejeli Bokono kwa ubinafsi
wake na kuwanyanyasa wanabutangi.
Kaloo anaingia uwanjani kwa kutayarisha ,anamwona
Mwelusi na anadhani ni mmoja wa waliohudhuria lakini Mwelusi anamwambia alikuwa
anapita tu ni mawazo yaliyomshika mguu.Kaloo anafurahi kwa kuwa
Mwelusi anawaza juu ya Butangi si kama vijana wengine wanavyo waza kuhusu
anasa. Mwelusi anakubaliana naye na kuongeza kuwa ni wakati wa vita. Kaloo
hakubaliani naye na anamuomba amfafanulie matamshi yake. Mwelusi anamwambia
kuwa atamueleza siku nyingine kwa kuwa hahudhurii mkutano na anaondoka.
Mwelusi Batu anaingia kuukagua uwanja, anafurahishwa
na viti.Anapoelezwa kuwa Mbutwe seremala aliyeunda viti anadai kulipwa Batu
anasema aje amwone na amdai malipo ya mbuzi wawili.
Wanawake ndio watakaocheza katika mkutanowa Bokono
Mtemi wa Butangi.Batu anasema kuwa mtemi akifurahi,wanawake watafurahi.Azenaanaingia
uwanjani ili kumsaidia kaloo kwa matayarisho.
Batu anaapoondoka Atega anaingia akifuatwa na
Mwelusi. Wanashukiwa kuwa wapenzi kwa kuwa kila mara wanaonekana pamoja.Naye kama
Mwelusi, anawafahamisha hatohudhuria mkutano.Batu anaingia tena
uwanjani na kuamrisha watu waitwe.Gege anaingia uwanjani huku akiwa
anapuliza ala ya muziki. Batu anamwambia ni muziki wa kuvutia, yeye anasema
kuwa anausifia uongozi wa busara wa Butangi. Kaloo anamhakikishai kuwa yeye na
jamaa zake ni wazalendo kamili na hawatasita kuhudhuria mkutano.
Batu anawasaidia kujitayarisha jinsi watamsifia
Bokono;Bokono Bokono milele!!
Baada ya muda kidogo wanagundua kuwa watu hawaji
kwa mkutano.Kalooanaenda Mingamiwili na kurudi lakini hakuwapata watu huko
pia.
Bokono anapofika anapata hakuna watu kwa uwanja
anakasirika sana. Vibaraka wake wanamuahidi kuwa kuna tatizo lakini
watalinyoosha. Zigu anasema kuwa watu wamechochewa na Mwelusi.Hata hivyo
Batu anasema kuwa watamkomesha anayewachochea watu.Baada ya mabo
kutulia wote wanaanza kumsifia Bokono ;Utaongoza Butangi kwa miaka mia moja.
Onyesho la pili
Matukio ni katika makazi ya Mtemi Bokono
amabayo ni sehemu ya majengo ya Utawala wa Butangi.Bokono amesimama huku
akiangalia vitu vilivyo ukutani na mara kwa mara anaguza hiki na kile.mkewe Nyalwe
amekaa kitini raha mustarehe, akjipepea.punde Mgezi anakuja hadi
alipo Nyalwe na kumuambia kuwa chakula kiko tayari.
Wanapokaa kula Bokono hali chakula ana wasiwasi sana.
Nyalwe anapomuuliza ni kwa nini hali anamjibu kwa kejeli na kumuuliza juu ya
vyeo vyake;mke, mwndani na msiri wake.
Nyalwe anamueleza Bokono kuhusu ndoto yake .Bokono
anakubali kuwa ana hofu ya kunyang’anywa utawala.Nyalwe anamuomba abadilishe
mienendo yake na anamuonya dhidi ya vibaraka wake wanoandanganya kuwa anapendwa
na Wanabutangi.
Bokono anapiga nduru kuwa amamwona nyoka ,anasema
ameumwa na bafe lakini wanagundua kuwa hamna nyoka mle ndani ni hofu tu ya
Bokono.
Nyalwe anampa Bokono habari kuhusu kijiji cha Mama
Agoro ambao wangependa kuwagawia huzuni.Hii ni baada ya uwanja wao wa
watoto kuchezea umepewa Askari mkuu.Mama Agoro aliahidi kuridi tena
na tena kutetea haki yao.
Onyesho la tatu
Onyeshao hili ni katika gereza. Gereza ni chumba
chenye kidirisha kimoja, kuta na sakafu chafu.
Tunaonyeshwa mateso na dhuluma kwa Mwelusi kutoka
kwa Mweke na Talui.
Wanaanza kwa kumita mtukufu mtemi anaponyamaza
wanazidi kunchapa na kumsukuma hapa na pale.
Mwelusi analalamika kuwa taya zake zinawaka moto
kwani waliodai wamekuja kuzungumza naye wanafanya hivyo kwa mateke na makofi.
Wanamhoji Mwelusi na kumuuliza kama yeye ni mwelisi
wa Biuki na kama anatoka kijiji cha Bunyanya na ukoo wa langile.Anapojibu
wanamsifu kuwa yeye ni muungwana na ni kiongozi mzuri sana wa Butangi.
Wanamuuliza kama yeye ndiye kiongozi wa kundi la
kabakaba.Wanazidi kumchapa ili aliri kuwa anahusika na shughuli za ukombozi
lakini Mwelusi anakataa wanazidi kumachapa.
Batu anaingia na kuwakataza kumchapa, anaomba nafasi
azungumze na Mwelusi.
Kwa upole anamshawishi Mwelusi akiri kuwa kiongozi
wa wanamapinduzi na aombe msama kwa Mtemi Bokono.
Mwelusi anapolia juu ya maumivu Batu anamwambia kuwa
atapewa dawa nzuri akitoka gerezani baada ya kuomba msamaha.Batu anamuacha
mwelusi peke yake kwani anadai kuwa akili ya binadamu hufanya kazi vizuri akiwa
peke yake. Anaporudi na kupata welusi hajafanya uamuzi .
Antaka akiri kwamba anatumiwa na majirani ili
kuchafua Butangi. Anapotataa Btu anamwambia kuwa amepotoshwa . Batu anatoa
ishara kwa Askari na kuondoka.
Sura ya nne
Onyesho hili linatokea mbele ya gereza.Andua amemletea
ndugu yake chakula.Askari wanamkataza kumuona na Askari 111 anajaribu
kumdhurumu.Askari wanapanga kula chakula cha mfungwa lakini askari 1
anawakataza na kuwaomba wampe mfunwa chakula chake.anawaambia wenzake kuwa ni
walafi.wanazungumza kuhusu utawala wa mtemi Bokono kama utafikia kilele au la.
Askari 11 anaeleza jinsi walijaribu kumgeuza
mhutumiwa Fulani aache kuwa jiwe awe binadamu.Walimng’oa kucha za mkono na za
miguu, walimgeuza kuwa popo na baadaye walifika katikati ya miguu yake na
kupiga kambi hapo.badaye walimuua na kumzika msituni.
Onyesho la tano.
Onyesho hili ni nyumbani kwa Tanyauani.Tanya ameketi
akidondoa nafaka katika uteo.Kwenye sehemu nyingine ya ua Gege amekaakaribu na
uzio akiukaguakagua.punde anauachilia na kuanza kujishughulisha
na utengenezaji wa ala ya muziki.
Mamake anamuuliza kwa nini hajaenda kumtizama
nduguye, Mwelusi kule gerezani.Gege anwambia mamayake
asimzomee.Anaendelea kutengeneza ala na kusema kuwa wasichana watamtambua .
Katika kumbukumbu zake Mwelusi anarejea na kumuuliza
hali ya uwnaja wa ngoma. Wazungumza kuhusu hali ya wanabutangi.Gege anamshuritisha
nduguye kwa kujali jamii kila mara na kusahau maisha yake mwenyewe. Mwelusi
anamuomba aieonee huruma Butangi na awe mzalendao.
Andua anarejea nyumbani kutoka kisimani.Anajeraha
upande mmoja wa uso wake.Anamueleza mam yake kuwa hakupigana mbali amechapwa na
Askari.
Azena anawatemebelea na kumtuliza Tanay juu ya
mwanawe.Anamuomba asife moyo na azidi kumpelekea chakula.
Onyesho la sita
Onyesho hili ni nje ya gereza pia. Tanya
amamletea Mwelusi chakula na pia anataka kuonana naye.Askari wanchukua chakula
na kuahidi kuwa watampelekea. Tanya anapowaomba Askari kumwona mwanawe Askari
11 na 111 wanamkazata. Askari 1 anamuhurumia Tanya na kuwaomba wenzake
wamkubalie mama huyo kumwona mwanawe.
Baadaye Atega analeta chakula zaidi cha mfungwa
pamoja na tembo.Askari wanakula chakula hiki na Kumuomba askari 1 ampelekee
rafiki yake mkate wa wishwa.
Askari 1 anawahadithia juu ya Makea na ulevi wake.Muda huu
wote Mwelusi amekuwa akikata minyororo kwa tupa.
Baadaye askari 111 napoenda kuchungulia anamwona na
kumwita mwenzake atazame pia.Muda kidogo wanasikia umati wa watu
.askari wote wanapotea Mwelusi anafunguliw gereza na kupotea.
Onyesho la saba
Matukio ya onyesho hili ni katika ukumbi wa
utawala wa Butangi.Kunamkutano kati ya Bokono na vibaraka wake.Lengo la
mkutano huu ni kupata suluhu la Mwelusi na uchochezi wake.
Kame anasema wamuachilie lakini batu anasema
hawawezi kumwachilia mhuni.Maoni yake ni kuwa Mwelusi anafaa kuuliwa.Batu anasema
kuwa wawandanganye watu kuwa Mwelusi amkufa juu ya ugonjwa wa moyo au aachiliwe
kasha njiani apigwe pembe na nyati.Kame anpinga wazo la kumwaga damu
ya binadamu.
Askari 11 naingia na kuwaarifu kuwa Mwelusi
amatoroka gerezani.anapoomba msamaha Batu anamuonya kuwa lazima wamtafute
Mwelusi na waijaribu kutoroka kutoka Butangi.
Bokono anajiunga nao na anaposikia habari za
kutoroka kwa Mwelusi anakasirika na anawaomba wampe heshima yake. Baadaya
anawaomba vibaraka wake au wazee wamtafute na kumuua.
Batu anatumia Mweke na Talui kumshawishi
Gege.Anamwambia amlete pale na kumshawishi.Mweke na Talui wanafanya
walivyo ambiwa na Kumwahidi Gege ndoa na Alida baada ya kumuua
Mwelusi.Wanajifanya wao ni wavuvi wawili na kuhadithi juu ya ndoa ya Gege na
Alida.
Onyesho la nane
Onyesho ni uani kwa Tanya.Tanya anajishughulisha
na kazi za nyumbani.Batuanaingia na kumsalimu.Baada yakuamkiana
batu anamwambia kuwa amakuja kwa ziara ya kirafiki. Sitiari ya kozi na
njiwa inatolewa na Tanya.Batu anaulizia kuhusu Mwelusi .Hii ndio
sababu yake kuja kwa Tanya.
Azena anaingia huku akitembea kwa shida.Anasema
jinsi walivyovamiwa na mali yao yote kuchomwa.Batu anasema kuwa ni
majirani wao waliowavamia lakini azena anasema kuwa ni uongo walivamiwa na
wahini wa kulipwa na kina Batu.
Tanya na Azena wanajikumbusha nyimbo walizomuimbia
Bokono.
Mwelusi ana Atega wanatokea na kwa kutumia shingo
Tanya anawaelekeza watoroke.Baada ya Batu kutoweka Mwelusi anaeleza
mama yake alivyookolewa na umati.
Askari wanakuja kwa fujo lakini Mwelusi na Atega
wanfaulu kutoroka.
Kame anakuja pia na kufikia sasa Tanya anamkejeli
kuwa utawala wa Butangi umemtembelea imebaki Bokono Mwenyewe.Kame anawaeleza
kuwa nyoyo zao ziko pamoja nay eye ni mmoja wa wanamapindizi.Wote wanaondoka
kuelekea kisima cha mkomani aliko Andua na wanamapinduzi wengine.
Onyesho la tisa
Matukio ya onyesho hili ni kisima cha Mkomani.Ni asubuhi
na zigu amesimama huku macho yake yakilikagua bonde.Kaloo anatokea na
anapofika karibu na zigu zigu anashtuka.zigu anamuulizia kaloo
kuhusu maoni ya wanakijiji wnzake juu ya kannuni mpya
zilizotangazwa.Anasema kuwa kanuni zote za Butangi ni za busara.
Kaloo anamtuma zigu amshukuru Bokono Kaloo anamtuma
zigu amshukuruBokono kwa ajili ya kazi aliyoamuru mototo wake apewe.kaloo hajali
juu ya Butangi yeye anataka awe na uhusiano na Bokono ili apate mali zaidi.Kaloo anaambiwa
kuwa ni vyema aende akamshukuru mwenyewe kwani hivi karibuni Bokona amekuwa
akimtaja mara kwa mara.
Andua anapokuta kuteka maji zigu anamkataza na
kumueleza kuhusu kanuni.baadaye Mwelusi na Atega wanatokea lakini Zigu
hawatambui.Anawazungumzia kuhusu Mwelusi aliye gerezani.Zigu ako
tayari kutetea kanuni za Butangi hata kwa silaha.
Baadaye Gege anakuja na kumdanganya Mwelusi kuwa
ametumwa na mama yao Tanya huku akilia , ni ujumbe muhimu ambazo babayao
alimwachia. Wanaenda chemba na Gege anamuua.Kame anafika
amechelewa na wote wankimbia chemba baada kusikia sauti yenye huzuni.
Onyesho la kumi
Matukio ya onyesho hili ni katika Ukumbi wa Utawala
wa Butangi.Kiti cha mtemi kiko mahali pake,lakini ni kitupu.Batu ymo ukumbini.Punde Mweke
anaingia na baadaye Gege. Wakati Gege anadai malipo yake Baada ya kumuua
Mwelusi ndio anagundua kuwa alidanganywa.Batu anamwahidi kuwa atapata
zawadi ya ardhi.Bokono anapoingia anamwahidi kuwa atapewa jina Mkuki wa Almasi.
Nyalwe anaingia kwa wasiwasi na kuwaonya kuwa
umati wa watu unakuja.wanampuuza.Hata hivyo wanashangaa kuwa Mweke
hajaleta habari zozote na Zigu pia hakuweko.
Azena anaingia ukumbini kama ameinua panga.Kisha askari1,Kame
na Atega.Atega anamtetea nyalwe asifungwe kwani alikuwa kamwe
anatetea Wanabutangi.Wanawafunga Bokono, Batu,Gege na kuwatoa nje .Watu
wanasherekea ukombozi wao.
WAHUSIKA
Wahusika ni binadamu wa kawaida na wanaendeleza
shughuli za kawaida za kila siku za binadamu.
Mhusika mkuu ni Mwelusi .Ni
kiongozi katika shughuli za ukombozi wa butangi.Anafungwa katika jela na
kuteswa sana.(uk 21) onyesho la tatu.
Gege ni
nduguye Mwelusi yeye anaendleza maudhui ya ubinafsi.Hana utu,ni
msaliti na pia muuaji kwani alimmuua Mwelusi pale kisimani.
Bokono ni
kiongozi mbaya mwenye udikteta.Ananyanyasa na kukandamiza
Wanabutangi.Anawanyima wanabutangi haki zao Kupitia vibara wake Batu na
Zigu.Viongozi hawa ni wakatili,hawana utu. Wanamdanganya Bokono kwamba
anapendwa lakini huo ni unafiki wao.
Tanya na Azena ni
wanawake wanao tetea haki za wanabutangi.Tanya ni Mamake mwelusi na
nimkakamavu anazozana na Batu na habadilish msimamo wake.Uk 76
onyesho la nane.
Atega na Andua ni
wasichana ambao wanashiriki katika ukombozi ni wakamavu, wana ujasiri na pia ni
wenye nidhamu hasa Atega kwa kuwapa askari tembo na kumpelekea Mwelusi tupa.Hawa ni
wahusika wasaidizi.
Kuna wahusika wengi kama vile Askari 11
na 111ambao wanaendeleza maudhui ya ukatili na dhuluma pamoja na Mweke
na Talui.
Kame na Askari
1 ni wenye utu na wamezinduka na kushiriki katika ukombozi.
Kaloo ni
kibaraka wa Mtemi Bokono.Yeye hajazinduka.Ni mwenye ubinafsi na
anamtetea mwanawe.Ni mfisadi
MANTHARI
Ni mahali au mazingira yanayotumika katika kitabu.
Mazingira ya kawaida yametumika katika tamthilia hii.Kuna mazingira
ya kinyumbani kama vile Kwa Tanya, Nyumbani kwa Bokono uk 12 onyesho la pili.Kuna mazingira
ya uwanjani, kisimani na gereza.
MBINU ZA UANDISHI NA ZA LUGHA
Kejeli uk
21 Mweke na Talui wanawita Mwelusi Mtukufu Mtemi.Hii ni kejeli kwani
Mwelusi si mtemi mbali ni kiongozi wa ukombozi.Kejeli inasaidia kuendeleza
maudhui ya dhuluma.
Matumizi ya Ndoto uk 14 Nyalwe
mkewe Bokono antuhadithia jinsi usiku mmewe alikuwa akiota na kusema watu
wamtoe kaburini. Ndoto hii inaonyesha hofu ya Bokono kutokana na utawa wake
ambao ni mbaya.Ndoto hii inaendeleza maudhui ya Hofu na utamaushi.
Kuna Nyimbo uk 81Azena na Tanya
wanakumbuka nyimbo za kumsifia Bokono. Wimbo huu unaonyesha Bokono kama
kiongozi bora asiye na kasoro.Wanabutangi waliimuinua Bokono karibu na
mungu.Maudhui yake ni ya uongozi wa kidkteta.
Kuna matumizi ya Taswira.Hizi ni picha
zinazojengeka katika akili ya msomaji.Mwandishi ametumia taswira mbalimbali
kama vile gereza.Uk 21 gereza imechorwa kama mahali penye kidirisha
kimoja ,kuta na sakafu chafu. Picha hii inasaidia kuendeleza maudhui ya dhuluma
na kunyimwa haki kwa mfungwa.
Takriri imetumika
uk 6 ambapo Kaloo, Azena na Gege wanakariri Bokono Bokono Milele mara kadhaa.Hii inasaidia
kumpa Bokono matumaini ya kuwa anapendwa.Huu ni Unafiki.Kuna takrir
pia katika kurasa zifuatazo uk 8,11,14
Tashhisi imetumika
katika ukurasa wa kwanza ambapo sauti inasema kuwa jua lina bahati,jua lina
uwezo uwezo mkubwa. Mwelusi pia anasema mawazo yamemshika miguu kuonyesha hofu
aliyonayo.askari wanasema kuwa siku inajikokota. Uk 53.Hii inaonyesa ukatili
wao na dhuluma na mateso wanayomletea mwelusi. Andua anaambiwa na Askari
asipoondoka atatemebelewa na makofi.Hii ni dhuluma.
Tashbihi ni
ulinganisho wa moja kwa moja wa vitu au watu na wanyama. Mfano uk71Alida
bintiye mtemi ana shingo ya upanga.Hii ni kusaidia kumshawishi Gege
na maelezo haya yanaendeleza unafiki kwani ndoa anayoahidiwa na hurulaini
haipo. Uk 37 Askari wanasema uharibifu wa mwelusi uko wazi kama meno ya ngiri.
Jazanda ni
picha inayomwingia mtu akilini na kuilinganisha na hali ya kawaida.Mfano uk
61 Batu anaashiriwa kama macho na masikio ya Butangi, uk64 mwelusi ni mwiba
wa Butangi.Hii ni tofauti na jukumu lake la kuleta mabadiliko katika
utawala wa Butangi lakini si kuzuuia maendeleo.
Methali mfano
uk55 Batu anasema kuwa dawa ya moto ni moto. Hii ni katika hatua aliyochukua ya
kutumia watu kuvamia kina Azena.Huu ni ukatili wa kiwango cha juu.
Methali pia zimetumika katika kurasa zifuatazo 16,52,39,102 na kadhalika
Chuku ni
kutia chumvi au kuongeza sifa ili jambo au kitu kiwe cha kuvutia. Mfano uk 71
Maelezo ya Alida yametiwa chumvi ili kumvutia Gege.
Katika uk 9 baada ya mambo kutulia na hasira ya
mtemi Bokono Kuisha Batu,Zigu,Kaloo, Azena na wengine waliofika wanaanza
kumsifia Bokono ;Utaongoza Butangi kwa miaka mia moja.Hii ni chuku
kwani Mtemi ameshazeeka na hawezi kutawala kwa miaka mia moja.
Chuku pia imetumika katika kurasa zifuatazo
30,72,56 na kadhalika.
Semi uk27
Mwelusi anasema koo lake liko motoni.Hii ni baada ya kichapo na
mateso anayopata gerezani.Semi hii imetumika kuonyesha dhuluma na
mateso kwa Mwelusi. Askari 11 anaeleza jinsi walijaribu kumgeuza mhutumiwa
Fulani aache kuwa jiwe awe binadamu.Walimng’oa kucha za mkono na za miguu,
walimgeuza kuwa popo na baadaye walifika katikati ya miguu yake na kupiga kambi
hapo.Inamaanisha kuwa walimvuta na kumkata na kumdhulumu sehemu zake za siri.
Semi pia zimetumika katika kurasa zifuatazo 15.27,37
na kadhalika
Mwandishi ametumia Lugha ya Matusi. Hasa
katika mazungumzo ya Bokono na Nyalwe.Mfano mwehu
MAUDHUI
Mambo muhimu yanayoelezwa katika tamthilia.Mwandishi
ameshighulikia maudhu kuu kama vile uongozi mbaya, dhuluma na
mateso,ubinafsi na ukombozi.maudhui mengine ni kama vile usaliti, ubinafsi,
utu, unafiki na uchochezi.
Uongozi Mbaya
Mtemi wa Butangi Bokono pamoja na vibaraka
wake Batu na Zigu wanaendeleza maudhui ya uongozi mbaya. Wanamfanya Mwelusi
kukamatwa na kufungwa gerezani bila makosa yoyote amabayo wanaweza
kuthibitisha.
Katika Mkutano batu anaeleza jinsi walichoma kijiji
cha Kina Azena na kusema mfumo wake wa uongoni ni dawa ya moto ni moto.
Kwa kuwa Mwelusi anatetea haki za wanyonge Bokono
anamwita mwiba. Hii ni kwa sababu anazuia yeye na vibaraka wake
kujichumia mali. Mwishowe wanamtumia Gege kumuua.
Wanaamua kuwanyima Wanabutangi haki ya kuteka maji
pale kisimani. Mtemi anauliza kamawamewatangazia watu kuhusu kanuni mpya ya
kuteka maji kisima cha Mkuyuni kuwa ni siku tatu kwa wiki.
Dhuluma Na Mateso
Askari 11 anaeleza jinsi walijaribu kumgeuza
mhutumiwa Fulani aache kuwa jiwe awe binadamu.Walimng’oa kucha za mkono na za
miguu, walimgeuza kuwa popo na baadaye walifika katikati ya miguu yake na
kupiga kambi hapo.badaye walimuua na kumzika msituni.uk 43
Mwelusi anafungwa gerezani kama hakuna kesi na hajahukumiwa.Batuanapomtemebela
baada ya kumshawishi akiri kutochochea Wanabutangi na kushindwa anawaagiza
Askari wazidi kumchapa na kumtesa.uk 29
Katika uk 30 Mwelusi anasema anachomwa na mikuki mia
moja na anaelezwa kama anayeumia.Hii ni kutokana na kichapo
anachopata kutoka kwa Askari.
Uk49 Andua anasema kuwa hakupigana alipigwa na ndia
sababu ako na jeraha upande mmoja wa uso wake.Anasema kuwa ni Ni Askari
waliwapiga kule kisima cha Mkuyuni baada ya wao kwenda kuteka maji.
Askari wa Butangi kulingana na Tanya si wa kulinda
mbali ni wa kuleta mateso na kuwachapa Wana butnagi. Tanya anasema kuwa juzi
walimngoa motto wa Chendeke meno.
Uk 24 Mweke na Talui wanapokuja kuzungumza na
Mwelusi wanafanya hivyo kwa makofi na mateka.Mwelusi anasema kuwa taya zake
zinawaka moto.
Batu anajaribu kuukinga uongozi wa Bokono na
amamuomba mwelusi kuacha uchochezi na kuomba msamaha.Mwelusi anapokataa kukiri
kwamba anatumiwa na majirani ili kuchafua Butangi. Anapotataa Batu anamwambia
kuwa amepotoshwa . Batu anatoa ishara kwa Askari na kuondoka. Yeye anawpa
ruhusa Askari wamtese mwelusi badala ya kumlinda.uk 36
Ubinafsi
Tunauona ubinafsi wa Gege .Uk wa 95 Gege anamuua
Mwelusi nduguye ili apate kuozwa Alida bintiye Mtemi. Uk 17 anamuambia Mwelusi
ajali maisha yake aachane na jamii. Gege hajali maisha ya wnabutangi wengine
anajijali yeye mwenyewe.
Uk 89 Kaloo anamtuma zigu kwa Bokono amshukuru kwa
ajili ya kazi aliyoamuru mototo wake apewe.kaloo pia hajali juu ya
Butangi yeye anataka awe na uhusiano na Bokono ili apate mali zaidi.
Gege hajaenda kumtizama nduguye, Mwelusi kule gerezani.Gege anwambia
mamayake asimzomee anapoulizwa.Anaendelea kutengeneza ala na kusema kuwa
wasichana watamtambua .Hivyo anajali sana wasichana kuliko nduguye.uk43
Ukombozi
Mwelusi,Atega.Andua,Kame na Askari 1 ni baadhi
ya wanamapinduzi katka Butangi.
Watu hawa wanapinga utawala wa Mtemi Bokono na
vibaraka wake.
Wakati Mwelusi amefungwa gerezani Atega anamletea
mkate wa wishwa ukiwa na tupa ambayo anatumia kukata minyororo na kujikomboa.
Baadaye umati wa watu wanakuja na kumsaidia kufungua gereza na kujikomboa.uk 59
Kwa Uongozi wa Mwelusi wanaendelea kutetea
haki zao.Mfano Andua anaenda kisimani kuteka maji.
Hata baada ya mwelusi kuuliwa na Gege wanamapinduzi
hawa wanaendelea na harakati zao za ukombozi. Uk 105
Kitabu kinaisha kama Bokono,Batu,Zigu , Mweke na
Gege wamefungwa kamba baada ya kufumaniwa na Waandamanaji.Hivyo wanaukombozi
wanafaulu kukomboa Butangi kutokana na utawala Mbaya.
Mwelusi anadaiwa kuwa yeye ndiye kiongozi wa
kundi la kabakaba. Anahusika na shughuli za ukombozi.Ni yeye kiongozi
wa kundi hili la wanamapinduzi.
Usaliti
Gege anamsaliti kakake, Mwelusi kwa Kumuua
pale Kisimani. Uk 95 Gege anamdanganya Mwelusi kuwa ametumwa na mama yao Tanya
huku akilia , ni ujumbe muhimu ambazo babayao alimwachia. Wanaenda chemba
na Gege anamuua.
Viongozi wa Butangi ikiwemo Batu na Zigu
wanawasaliti kwa kuwanyima haki zao na kuwatesa.
Utu
Kame Askari 1 ni wenye utu wanamtetea Mwelusi.
Uk 60 wakati Batu na zigu wanataka kumuua Mwelusi
Kama anasema wamuachiliea kwa kuwa hana makosa yoyote.
Uk 35 Tanya anapowaomba Askari kumwona mwanawe
Askari 11 na 111 wanamkazata. Askari 1 anamuhurumia Tanya na kuwaomba wenzake
wamkubalie mama huyo kumwona mwanawe.
Hawa wawili paoja na wengine kama vile Azena na
Atega ni wenye utu miongoni mwa wanabutangi wengi ambao wana unyama kama vile
Batu.
Askari wanapanga kula chakula cha mfungwa lakini
Askari 1 anawakataza na kuwaomba wampe mfunwa chakula chake.uk 37
Unafiki
Uk 25 Mweke na Talui wanamhadithia Gege jinsi harusi
yake na Alida itakavyokuwa. Wanamwambia Gege amuue Nduguye Mwelusi na atapewa
mali pamoja na kuoa mtotot wa Mtemi Bokono.
Wakati Gege anaenda kudai malipo yake Baada ya
kumuua Mwelusi ndio anagundua kuwa alidanganywa.Talui na Mweke ni
wanafiki walijua kuwa wanamdanganya Gege ili awasidie tu kumumaliza Mwelusi.
Batu anapomtemebelea Mwelusi gerezani anamwambi a
kuwa ni rafiki yake na kumuomba ajiunge naye katika kuitumikia Butnangi.Huu ni
unafiki kwani kabla ya hapo alipokuwa kwenye mkutano na Zigu na Kame alpanga
jinsi watakavyo muua.
Uk 79 Batu anapomtembelea Tanya anamwita
rafiki yake tangu ujana wao.huuni unafiki kwani Batu yuko pale kumtafuta
Mwelusi.
Baada ya kumuahidi Tanya kuwa watampa Mwelusi chakula
Askari wanakula chakula hiki na Kumuomba askari 1 ampelekee rafiki yake mkate
wa wishwa. Uk 58. Huu ni unafiki.
Uchochezi
Kabla mkutano uanze Mwelusi anafika pale na
kudai kuwa anapita.Hata hivyo nia yake wakiwa na Atega ni kuwachochea
watu wasuhudhurie mkutano wa Mtemi Bokono.Uk 1
Uk wa 9 Zigu anasema kuwa kuna fununu ya kuwa kuna
kijana anayechochea watu.Kijana huyu ni Mwelusi.
Uk 90 Zigu anamwambia Kaloo kwamba Bokono amekuwa
akimtaja mara kwa mara.Zigu ananchochea Kaloo aonane na Bokono na
kumpa shukrani yeye mwenye kwa kazi ambayo Bokono alamuru motto wa Kaloo apewe.
FALSAFA YA MWANDISHI
Mwandishi analenga kuzindua wananchi kuhusu utawala
mbaya.Anatetea haki za walionyanyaswa na kukandamizwa. Anashikila kuwa kuna
uwezo wa kujikomboa kutoka kwa uongozi mbaya .Hii ni kupitia kwa watu kuungana
na kuandama na kutetea haki zao na kubadilisha uongozi mbaya ,pamoja na
kuwafungaviongozi wabaya.
Falsafa ya Kithaka ni haki na hukumu kwa wenye
makosa.
NADHARIA
Mwandishi ametumia Nadharia kama vile Umaksi.Katika
Butangi wenye mali wananyanyasa wasio na mali.Kuna Ufeministi kwani
Atega ,Andua Tanya na Azena ni wahusika wa kike wanaoshiriki katika ukombozi.Kuna Uhalisia Kwani
matukio ni ya kawaida kam vile uongozi mbaya na kunyimwa haki katika maisha ya
kila siku. Kuna Utamaushi kwani wanabutangi wamekata tama.MfanoTanya
anamtaka Mwelusi aondoke Butangi
HITIMISHO
Mwandishi amefaulu kutumia mbinu na kutoa maudhui
kwa kutumia nadharia. Kithaka anatetea haki kwa wenye Kunyanyaswa na hukumu kwa
wenye makosa.Amewatumia wahusika wa kawaida kuutoa ujumbe wake.
Kuna udhaifu katika anwani kwani sio wahusika wote
wanaathiriwa na kifo kisimani.Kitabu kimeshughulikia zaidi ya kifo.
UHUSIANO KATI YA TAMTHILIA YA KIFO
KISIMANI NA UTENZI W A FUMO LIYONGO
Utenzi wa fumo liyongo unamhusu shujaa Liyongo
kutoka jamii ya waswahili.liyongo alishuhudiwa na jamii yake na makabila jirani
kama vile wagalla.
Hata hivyo mfalme wa pate(Daudi Mringwari)
alimchukia kwa kuhofu kuwa angemnyang’anya utawa wake.Hivyo alipanga
njama za kumwangamiza liyong.Akamtia gerezani alikolindwa na Askari wake.Akiwa gerezani,
aliletewa mkate wa wishwa uliotiwa tupa.Aliitumia tupa hii kukata minyororo
kasha akotoroka.
Mfalme wa pate hakukata tama.Alimshawishi mwanawe
Liyongo kumuua babake na kumwahidi kumwoza bintiye.Liyongo akauliwa na mwanawe
kwa kumfuma msumari wa shaba kitovuni.Liyongo alifia kisimani na kuwatisha watu
wasichote maji kwa siku kadhaa.
Utenzi huu kwa kiasi kikubwa unahusiana na tamthilia
ya Kifo Kisimani, inayomhusu Mwelusi anayepinga utawala dhalimu wa Mtemi
Bokono. Anachukiwa na Bokono pamoja na vibaraka wake kwa hofu kuwa atauangusha
utawala huo.Anatiwa gerezani lakini anatoroka baada ya kukata minyororo kwa
tupa iliyotiwa ndani ya mkate wa wishwa alioletewa na Atega. Bokono anamtumia
nduguye Mwelusi, Gege kumuua kwa kumdunga kisu pale kisimani. Gege
vilevile anaahidiwa na Mweke wakiwa na Talui kuwa ataozwa bintiye mtemi.Alida.
Hata hivyo kuna tofauti nyingi kati ya tungo hizi
mbili. Fumo Liyongo ni mhusika wa kihistoria, aliishi baina ya karne 15 na
16.Mwelusi naye ni mhusika wa kubuni.Fumo alikuwa na sifa za kiajabu
kama vile nguvu zilizokithiri, mpiganaji hodari aliyeshinda vita vingi, ukubwa uliopita
kiasi na uwezo wa kutambua mabo kabla hayajiri.Mwelusi hana sifa kaa hizi
zinazomtambuliasha kama mhusika wa kipekee.Vita anavyopigana si vya
silaha bali anapinga dhuluma na mateso kwa Wanabutangi.
MAREJELEO.
- Kithaka
wa Mberia, (2001) Kifo Kisimani, Marimba Publications limited,
Nairobi Kenya.
- Rocha
M.Chimera, (1998) Kiswahili; Past, Present and Future Horizons,Nairobi
University Press,.Nairobi.
Visit our website and leave your comment : https://freekcserevisionpapers.blogspot.com
ALSO OTHER BOOKS AVAILABLE
1. mwongozo wa Mwenda wazimu by Mbatiah
2. mwongozo wa Siku Njema by ken walibora
3. mwongozo kifo kisimani
+more dOWNLOAD APP FOR FREE'BRILLIANT LEARNERS'……………………………………………………………………………………………….
1 comment:
This is what is happening now in Kenya
Post a Comment