Thursday, January 24, 2019

MWONGOZO WA TAMTHILIA YA KIFO KISIMANI BY KITHAKA WA MBERIA


kenyatta university 
MWONGOZO WA TAMTHILIA YA KIFO KISIMANI BY KITHAKA WA MBERIA
Compiled by Amos Sifuna Barasa

student
31/1/2019


 Tamthilia ya Kifo Kisimani imeandikwa na kithaka wa Mberia. Toleo la kwanza la kitabu hiki ililikuwa mwaka wa 2001 na kina chapa nyingi hadi kufikia mwaka wa 2009.kimechapishwa na Marimba Publications Ltd.

BY AMOS SIFUNA BARASA, KENYATTA UNIVERSITY

TAMTHILIA YA KIFO KISIMANI
UTANGULIZI
Tamthilia ya Kifo Kisimani imeandikwa na kithaka wa Mberia. Toleo la kwanza la kitabu hiki ililikuwa mwaka wa 2001 na kina chapa nyingi hadi kufikia mwaka wa 2009.kimechapishwa na Marimba Publications Ltd.
Anwani
Anwani huwa ni jina la kitabu.Mwandishi amefaulu kutumia anwani’Kifo Kisimani’. Anwani hii inaashiria kifo cha Mwelusi pale kisimani alipouliwa na Gege.
Pia anwani hii inaashiria kifo cha Wanabutangi baada ya kukosa maji pale kisimani.Hii ni baada ya kanuni mpya za utekaji maji kutolewa amabazo ziliwanyima haki za kuteka maji. Maji ni uhai hivyo kupewa siku tatu za kuteka maji ni kunyimwa uhai yaani kifo.
Jalada
Jalada ni karatasi ngumu inayofunika kitabu ambapo jina la kitabu huandikwa.Katika tamthilia hii kuna picha ya mtu aliye na huzuni.Mtu huyu ni kama ako katika shimo. Hii inaashiria shimo la mateso ambalo Wanabutangi wametiwa na utawala mbaya wa Bokono na vibaraka wake.
Kuna picha inayoashiria machea.Hii inaonyesha matumaini kwa Wanabutangi baada ya Mwelusi na wenzake kuanza harakati za mabadiliko.Rangi inayotumika kwa picha ni ya udongo, kuashiria rotuba ya Butangi.

DHAMIRA YA MWANDISHI
Kiini cha jambo au habari iliyoandikwa na mwandishi.Katika Kifo Kisimani Kithaka wa Mberia ananuia kuamsha au kumchangamsha msomaji kuhusu utawala mbaya na jinsi ya kuleta mabadiliko na kuuondoa .
Mwandishi anatetea haki za walionyanyaswa.Hivyo lengo kuu la mwandishi ni kuzindua watu.
PLOTI
Huwa ni mtiririko wa matukio katika kitabu.Tamthilia hii ina onyesho kumi.Muhtasari wa onyesho hizi ni kama ifuatavyo.



Onyesho la kwanza
Mchezo unaanza asubuhi ambapo viti vimepangwa tayari kwa mkutano wa Bokono.Mwelusi ambaye ni kijan anaingia uwanjani.Mawazo yake yanadhihirika kupitia kwa sauti tunayosikia .Yanamkejeli Bokono kwa ubinafsi wake na kuwanyanyasa wanabutangi.
Kaloo anaingia uwanjani kwa kutayarisha ,anamwona Mwelusi na anadhani ni mmoja wa waliohudhuria lakini Mwelusi anamwambia alikuwa anapita tu ni mawazo yaliyomshika mguu.Kaloo anafurahi kwa kuwa Mwelusi anawaza juu ya Butangi si kama vijana wengine wanavyo waza kuhusu anasa. Mwelusi anakubaliana naye na kuongeza kuwa ni wakati wa vita. Kaloo hakubaliani naye na anamuomba amfafanulie matamshi yake. Mwelusi anamwambia kuwa atamueleza siku nyingine kwa kuwa hahudhurii mkutano na anaondoka.
Mwelusi Batu anaingia kuukagua uwanja, anafurahishwa na viti.Anapoelezwa kuwa Mbutwe seremala aliyeunda viti anadai kulipwa Batu anasema aje amwone na amdai malipo ya mbuzi wawili.
Wanawake ndio watakaocheza katika mkutanowa Bokono Mtemi wa Butangi.Batu anasema kuwa mtemi akifurahi,wanawake watafurahi.Azenaanaingia uwanjani ili kumsaidia kaloo kwa matayarisho.
Batu anaapoondoka Atega anaingia akifuatwa na Mwelusi. Wanashukiwa kuwa wapenzi kwa kuwa kila mara wanaonekana pamoja.Naye kama Mwelusi, anawafahamisha hatohudhuria mkutano.Batu anaingia tena uwanjani na kuamrisha watu waitwe.Gege anaingia uwanjani huku akiwa anapuliza ala ya muziki. Batu anamwambia ni muziki wa kuvutia, yeye anasema kuwa anausifia uongozi wa busara wa Butangi. Kaloo anamhakikishai kuwa yeye na jamaa zake ni wazalendo kamili na hawatasita kuhudhuria mkutano.
Batu anawasaidia kujitayarisha jinsi watamsifia Bokono;Bokono  Bokono milele!!
Baada ya muda kidogo wanagundua kuwa watu hawaji kwa mkutano.Kalooanaenda Mingamiwili na kurudi lakini hakuwapata watu huko pia.
Bokono anapofika anapata hakuna watu kwa uwanja anakasirika sana. Vibaraka wake wanamuahidi kuwa kuna tatizo lakini  watalinyoosha. Zigu anasema kuwa watu wamechochewa na Mwelusi.Hata hivyo Batu anasema kuwa watamkomesha anayewachochea watu.Baada ya mabo kutulia wote wanaanza kumsifia Bokono ;Utaongoza Butangi kwa miaka mia moja.




Onyesho la pili
 Matukio ni katika makazi ya Mtemi Bokono amabayo ni sehemu ya majengo ya Utawala wa Butangi.Bokono amesimama huku akiangalia vitu vilivyo ukutani na mara kwa mara anaguza hiki na kile.mkewe Nyalwe amekaa kitini raha mustarehe, akjipepea.punde Mgezi anakuja hadi alipo Nyalwe na kumuambia kuwa chakula kiko tayari.
Wanapokaa kula Bokono hali chakula ana wasiwasi sana. Nyalwe anapomuuliza ni kwa nini hali anamjibu kwa kejeli na kumuuliza juu ya vyeo vyake;mke, mwndani  na msiri wake.
Nyalwe anamueleza Bokono kuhusu ndoto yake .Bokono anakubali kuwa ana hofu ya kunyang’anywa utawala.Nyalwe anamuomba abadilishe mienendo yake na anamuonya dhidi ya vibaraka wake wanoandanganya kuwa anapendwa na Wanabutangi.
Bokono anapiga nduru kuwa amamwona nyoka ,anasema ameumwa na bafe lakini wanagundua kuwa hamna nyoka mle ndani ni hofu tu ya Bokono.
Nyalwe anampa Bokono habari kuhusu kijiji cha Mama Agoro ambao wangependa kuwagawia huzuni.Hii ni baada ya uwanja wao wa watoto kuchezea umepewa Askari mkuu.Mama Agoro aliahidi kuridi tena na tena kutetea haki yao.

Onyesho la tatu
Onyeshao hili ni katika gereza. Gereza ni chumba chenye kidirisha kimoja, kuta na sakafu chafu.
Tunaonyeshwa mateso na dhuluma kwa Mwelusi kutoka kwa Mweke na Talui.
Wanaanza kwa kumita mtukufu mtemi anaponyamaza wanazidi kunchapa na kumsukuma hapa na pale.
Mwelusi analalamika kuwa taya zake zinawaka moto kwani waliodai wamekuja kuzungumza naye wanafanya hivyo kwa mateke na makofi.
Wanamhoji Mwelusi na kumuuliza kama yeye ni mwelisi wa Biuki na kama anatoka kijiji cha Bunyanya na ukoo wa langile.Anapojibu wanamsifu kuwa yeye ni muungwana na ni kiongozi mzuri sana wa Butangi.
Wanamuuliza kama yeye ndiye kiongozi wa kundi la kabakaba.Wanazidi kumchapa ili aliri kuwa anahusika na shughuli za ukombozi lakini  Mwelusi anakataa wanazidi kumachapa.
Batu anaingia na kuwakataza kumchapa, anaomba nafasi azungumze na Mwelusi.
Kwa upole anamshawishi Mwelusi akiri kuwa kiongozi wa wanamapinduzi na aombe msama kwa Mtemi Bokono.
Mwelusi anapolia juu ya maumivu Batu anamwambia kuwa atapewa dawa nzuri akitoka gerezani baada ya kuomba msamaha.Batu anamuacha mwelusi peke yake kwani anadai kuwa akili ya binadamu hufanya kazi vizuri akiwa peke yake. Anaporudi na kupata welusi hajafanya uamuzi .
Antaka akiri kwamba anatumiwa na majirani ili kuchafua Butangi. Anapotataa Btu anamwambia kuwa amepotoshwa . Batu anatoa ishara kwa Askari na kuondoka.
Sura ya nne
Onyesho hili linatokea mbele ya gereza.Andua amemletea ndugu yake chakula.Askari wanamkataza kumuona na Askari 111 anajaribu kumdhurumu.Askari wanapanga kula chakula cha mfungwa  lakini askari 1 anawakataza na kuwaomba wampe mfunwa chakula chake.anawaambia wenzake kuwa ni walafi.wanazungumza kuhusu utawala wa mtemi Bokono kama utafikia kilele au la.
Askari 11 anaeleza jinsi walijaribu kumgeuza mhutumiwa Fulani aache kuwa jiwe awe binadamu.Walimng’oa kucha za mkono na za miguu, walimgeuza kuwa popo na baadaye walifika katikati ya miguu yake na kupiga kambi hapo.badaye walimuua na kumzika msituni.
Onyesho la tano.
Onyesho hili ni nyumbani kwa Tanyauani.Tanya ameketi akidondoa nafaka katika uteo.Kwenye sehemu nyingine ya ua Gege amekaakaribu na uzio akiukaguakagua.punde anauachilia na kuanza kujishughulisha  na utengenezaji wa ala ya muziki.
Mamake anamuuliza kwa nini hajaenda kumtizama nduguye, Mwelusi kule gerezani.Gege anwambia mamayake asimzomee.Anaendelea kutengeneza ala na kusema kuwa wasichana watamtambua .
Katika kumbukumbu zake Mwelusi anarejea na kumuuliza hali ya uwnaja wa ngoma. Wazungumza  kuhusu hali ya wanabutangi.Gege anamshuritisha nduguye kwa kujali jamii kila mara na kusahau maisha yake mwenyewe. Mwelusi anamuomba aieonee huruma Butangi na awe mzalendao.
Andua anarejea nyumbani kutoka kisimani.Anajeraha upande mmoja wa uso wake.Anamueleza mam yake kuwa hakupigana mbali amechapwa na Askari.
Azena anawatemebelea na kumtuliza Tanay juu ya mwanawe.Anamuomba asife moyo na azidi kumpelekea chakula.
Onyesho la sita
Onyesho hili  ni nje ya gereza pia. Tanya amamletea Mwelusi chakula na pia anataka kuonana naye.Askari wanchukua chakula na kuahidi kuwa watampelekea. Tanya anapowaomba Askari kumwona mwanawe Askari 11 na 111 wanamkazata. Askari 1 anamuhurumia Tanya na kuwaomba wenzake wamkubalie mama huyo kumwona mwanawe.
Baadaye Atega analeta chakula zaidi cha mfungwa pamoja na tembo.Askari wanakula chakula hiki na Kumuomba askari 1 ampelekee rafiki yake mkate wa wishwa.
Askari 1 anawahadithia juu ya Makea na ulevi wake.Muda huu wote Mwelusi amekuwa akikata minyororo kwa tupa.
Baadaye askari 111 napoenda kuchungulia anamwona na kumwita mwenzake atazame pia.Muda kidogo wanasikia umati wa watu .askari wote wanapotea Mwelusi anafunguliw gereza na kupotea.

Onyesho la saba
 Matukio ya onyesho hili ni katika ukumbi wa utawala wa Butangi.Kunamkutano kati ya Bokono na vibaraka wake.Lengo la mkutano huu ni kupata suluhu la Mwelusi na uchochezi wake.
Kame anasema wamuachilie lakini batu anasema hawawezi kumwachilia mhuni.Maoni yake ni kuwa Mwelusi anafaa kuuliwa.Batu anasema kuwa wawandanganye watu kuwa Mwelusi amkufa juu ya ugonjwa wa moyo au aachiliwe kasha njiani apigwe pembe na nyati.Kame anpinga wazo la kumwaga damu ya binadamu.
Askari 11 naingia na kuwaarifu kuwa Mwelusi amatoroka gerezani.anapoomba msamaha Batu anamuonya kuwa lazima wamtafute Mwelusi na waijaribu kutoroka kutoka Butangi.
Bokono anajiunga nao na anaposikia habari za kutoroka kwa Mwelusi anakasirika na anawaomba wampe heshima yake. Baadaya anawaomba vibaraka wake au wazee wamtafute na kumuua.
Batu anatumia Mweke na Talui kumshawishi Gege.Anamwambia amlete pale na kumshawishi.Mweke na Talui wanafanya walivyo ambiwa na Kumwahidi Gege ndoa na Alida baada ya kumuua Mwelusi.Wanajifanya wao ni wavuvi wawili na kuhadithi juu ya ndoa ya Gege na Alida.
Onyesho la nane
Onyesho ni uani kwa Tanya.Tanya anajishughulisha na kazi za nyumbani.Batuanaingia na kumsalimu.Baada yakuamkiana batu anamwambia kuwa amakuja kwa ziara ya kirafiki. Sitiari ya  kozi na njiwa inatolewa na Tanya.Batu anaulizia kuhusu Mwelusi .Hii ndio sababu yake kuja kwa Tanya.
Azena anaingia huku akitembea kwa shida.Anasema jinsi walivyovamiwa na mali yao yote kuchomwa.Batu anasema kuwa ni majirani wao waliowavamia lakini azena anasema kuwa ni uongo walivamiwa na wahini wa kulipwa na kina Batu.
Tanya na Azena wanajikumbusha nyimbo walizomuimbia Bokono.
Mwelusi ana Atega wanatokea na kwa kutumia shingo Tanya anawaelekeza watoroke.Baada ya Batu kutoweka Mwelusi anaeleza mama yake alivyookolewa na umati.
Askari wanakuja kwa fujo lakini Mwelusi na Atega wanfaulu kutoroka.
Kame anakuja pia na kufikia sasa Tanya anamkejeli kuwa utawala wa Butangi umemtembelea imebaki Bokono Mwenyewe.Kame anawaeleza kuwa nyoyo zao ziko pamoja nay eye ni mmoja wa wanamapindizi.Wote wanaondoka kuelekea kisima cha mkomani aliko Andua na wanamapinduzi wengine.

Onyesho la tisa
Matukio ya onyesho hili ni kisima cha Mkomani.Ni asubuhi na zigu amesimama huku macho yake yakilikagua bonde.Kaloo anatokea na anapofika karibu na zigu zigu anashtuka.zigu anamuulizia  kaloo kuhusu maoni ya wanakijiji wnzake juu ya  kannuni mpya zilizotangazwa.Anasema kuwa kanuni zote za Butangi ni za busara.
Kaloo anamtuma zigu amshukuru Bokono Kaloo anamtuma zigu amshukuruBokono kwa ajili ya kazi aliyoamuru mototo wake apewe.kaloo  hajali juu ya Butangi yeye anataka awe na uhusiano na Bokono ili apate mali zaidi.Kaloo anaambiwa kuwa ni vyema aende akamshukuru mwenyewe kwani hivi karibuni Bokona amekuwa akimtaja mara kwa mara.
Andua anapokuta kuteka maji zigu anamkataza na kumueleza kuhusu kanuni.baadaye Mwelusi na Atega wanatokea lakini Zigu hawatambui.Anawazungumzia kuhusu Mwelusi aliye gerezani.Zigu ako tayari kutetea kanuni za Butangi hata kwa silaha.
Baadaye Gege anakuja na kumdanganya Mwelusi kuwa ametumwa na mama yao Tanya huku akilia , ni ujumbe muhimu ambazo babayao alimwachia. Wanaenda chemba  na Gege anamuua.Kame anafika amechelewa na wote wankimbia chemba baada kusikia sauti yenye huzuni.

Onyesho la kumi
Matukio ya onyesho hili ni katika Ukumbi wa Utawala wa Butangi.Kiti cha mtemi kiko mahali pake,lakini ni kitupu.Batu ymo ukumbini.Punde Mweke anaingia na baadaye Gege. Wakati Gege anadai malipo yake Baada ya kumuua Mwelusi ndio anagundua kuwa alidanganywa.Batu anamwahidi kuwa atapata zawadi ya ardhi.Bokono anapoingia anamwahidi kuwa atapewa jina Mkuki wa Almasi.
Nyalwe anaingia kwa wasiwasi na kuwaonya  kuwa umati wa watu unakuja.wanampuuza.Hata hivyo wanashangaa kuwa Mweke hajaleta habari zozote na Zigu pia hakuweko.
Azena anaingia ukumbini kama ameinua panga.Kisha askari1,Kame na Atega.Atega anamtetea nyalwe asifungwe kwani alikuwa kamwe anatetea Wanabutangi.Wanawafunga Bokono, Batu,Gege na kuwatoa nje .Watu wanasherekea ukombozi wao.

WAHUSIKA
Wahusika ni binadamu wa kawaida na wanaendeleza shughuli za kawaida za kila siku za binadamu.
Mhusika mkuu ni Mwelusi .Ni kiongozi katika shughuli za ukombozi wa butangi.Anafungwa katika jela na kuteswa sana.(uk 21) onyesho la tatu.
Gege  ni nduguye Mwelusi yeye anaendleza maudhui ya ubinafsi.Hana utu,ni msaliti na pia muuaji kwani alimmuua Mwelusi pale kisimani.
Bokono ni kiongozi mbaya mwenye udikteta.Ananyanyasa na kukandamiza Wanabutangi.Anawanyima wanabutangi haki zao Kupitia vibara wake Batu na Zigu.Viongozi hawa ni wakatili,hawana utu. Wanamdanganya Bokono kwamba anapendwa lakini huo ni unafiki wao.
Tanya na Azena ni wanawake wanao tetea haki za wanabutangi.Tanya ni Mamake mwelusi na nimkakamavu anazozana na Batu na habadilish msimamo wake.Uk 76 onyesho la nane.
Atega na Andua  ni wasichana ambao wanashiriki katika ukombozi ni wakamavu, wana ujasiri na pia ni wenye nidhamu hasa Atega kwa kuwapa askari tembo na kumpelekea Mwelusi tupa.Hawa ni wahusika wasaidizi.
Kuna wahusika wengi kama vile Askari 11 na 111ambao wanaendeleza maudhui ya ukatili na dhuluma pamoja na Mweke na Talui.
Kame  na Askari 1  ni wenye utu na wamezinduka na kushiriki katika ukombozi.
Kaloo ni kibaraka wa Mtemi Bokono.Yeye hajazinduka.Ni mwenye ubinafsi na anamtetea mwanawe.Ni mfisadi

MANTHARI
Ni mahali au mazingira yanayotumika katika kitabu. Mazingira ya kawaida yametumika katika tamthilia hii.Kuna mazingira ya kinyumbani kama vile Kwa Tanya, Nyumbani kwa Bokono uk 12 onyesho la pili.Kuna mazingira ya  uwanjani, kisimani na gereza.

MBINU ZA UANDISHI NA ZA LUGHA
Kejeli uk 21 Mweke na Talui wanawita Mwelusi Mtukufu Mtemi.Hii ni kejeli kwani Mwelusi si mtemi mbali ni kiongozi wa ukombozi.Kejeli inasaidia kuendeleza maudhui ya dhuluma.
Matumizi ya Ndoto uk 14 Nyalwe mkewe Bokono antuhadithia jinsi usiku mmewe alikuwa akiota na kusema watu wamtoe kaburini. Ndoto hii inaonyesha hofu ya Bokono kutokana na utawa wake ambao ni mbaya.Ndoto hii inaendeleza maudhui ya Hofu na utamaushi.

Kuna Nyimbo uk 81Azena na Tanya wanakumbuka nyimbo za kumsifia Bokono. Wimbo huu unaonyesha Bokono kama kiongozi bora asiye na kasoro.Wanabutangi waliimuinua Bokono karibu na mungu.Maudhui yake ni ya uongozi wa kidkteta.
Kuna matumizi ya Taswira.Hizi ni picha zinazojengeka katika akili ya msomaji.Mwandishi ametumia taswira mbalimbali kama vile gereza.Uk 21 gereza imechorwa kama mahali penye kidirisha kimoja ,kuta na sakafu chafu. Picha hii inasaidia kuendeleza maudhui ya dhuluma na kunyimwa haki kwa mfungwa.
Takriri imetumika uk 6 ambapo Kaloo, Azena na Gege wanakariri Bokono Bokono Milele mara kadhaa.Hii inasaidia kumpa Bokono matumaini ya kuwa anapendwa.Huu ni Unafiki.Kuna takrir pia katika kurasa zifuatazo uk 8,11,14

Tashhisi  imetumika katika ukurasa wa kwanza ambapo sauti inasema kuwa jua lina bahati,jua lina uwezo uwezo mkubwa. Mwelusi pia anasema mawazo yamemshika miguu kuonyesha hofu aliyonayo.askari wanasema kuwa siku inajikokota. Uk 53.Hii inaonyesa ukatili wao na dhuluma na mateso wanayomletea mwelusi. Andua anaambiwa na Askari asipoondoka atatemebelewa na makofi.Hii ni dhuluma.
Tashbihi ni ulinganisho wa moja kwa moja wa vitu au watu na wanyama. Mfano uk71Alida bintiye mtemi ana shingo ya upanga.Hii ni kusaidia kumshawishi Gege na maelezo haya yanaendeleza unafiki kwani ndoa anayoahidiwa na hurulaini haipo. Uk 37 Askari wanasema uharibifu wa mwelusi uko wazi kama meno ya ngiri.
Jazanda ni picha inayomwingia mtu akilini na kuilinganisha na hali ya kawaida.Mfano uk 61 Batu anaashiriwa kama macho na masikio ya Butangi, uk64 mwelusi ni mwiba wa Butangi.Hii ni tofauti na jukumu lake la kuleta mabadiliko katika utawala wa Butangi lakini si kuzuuia maendeleo.
Methali mfano uk55 Batu anasema kuwa dawa ya moto ni moto. Hii ni katika hatua aliyochukua ya kutumia watu kuvamia kina Azena.Huu ni ukatili wa kiwango cha juu. Methali pia zimetumika katika kurasa zifuatazo 16,52,39,102 na kadhalika

Chuku ni kutia chumvi au kuongeza sifa ili jambo au kitu kiwe cha kuvutia. Mfano uk 71 Maelezo ya Alida yametiwa chumvi ili kumvutia Gege.
Katika uk 9 baada ya mambo kutulia na hasira ya mtemi Bokono Kuisha Batu,Zigu,Kaloo, Azena na wengine waliofika  wanaanza kumsifia Bokono ;Utaongoza Butangi kwa miaka mia moja.Hii ni chuku kwani Mtemi ameshazeeka na hawezi kutawala kwa miaka mia moja.
Chuku pia imetumika katika kurasa zifuatazo 30,72,56  na kadhalika.
Semi uk27 Mwelusi anasema koo lake liko motoni.Hii ni baada ya kichapo na mateso anayopata gerezani.Semi hii imetumika kuonyesha dhuluma na mateso kwa Mwelusi. Askari 11 anaeleza jinsi walijaribu kumgeuza mhutumiwa Fulani aache kuwa jiwe awe binadamu.Walimng’oa kucha za mkono na za miguu, walimgeuza kuwa popo na baadaye walifika katikati ya miguu yake na kupiga kambi hapo.Inamaanisha kuwa walimvuta na kumkata na kumdhulumu sehemu zake za siri.
Semi pia zimetumika katika kurasa zifuatazo 15.27,37 na kadhalika
Mwandishi ametumia Lugha ya Matusi. Hasa katika mazungumzo ya Bokono na Nyalwe.Mfano mwehu

MAUDHUI
Mambo muhimu yanayoelezwa katika tamthilia.Mwandishi ameshighulikia maudhu kuu  kama vile uongozi mbaya, dhuluma na mateso,ubinafsi na ukombozi.maudhui mengine ni kama vile usaliti, ubinafsi, utu, unafiki na uchochezi.
Uongozi Mbaya
 Mtemi wa Butangi Bokono pamoja na vibaraka wake Batu na Zigu wanaendeleza maudhui ya uongozi mbaya. Wanamfanya Mwelusi kukamatwa na kufungwa gerezani bila makosa yoyote amabayo wanaweza kuthibitisha.
Katika Mkutano batu anaeleza jinsi walichoma kijiji cha Kina Azena na kusema mfumo wake wa uongoni ni dawa ya moto ni moto.
Kwa kuwa Mwelusi anatetea haki za wanyonge Bokono anamwita mwiba. Hii ni kwa sababu  anazuia yeye na vibaraka wake kujichumia mali. Mwishowe wanamtumia Gege kumuua.
Wanaamua kuwanyima Wanabutangi haki ya kuteka maji pale kisimani. Mtemi anauliza kamawamewatangazia watu kuhusu kanuni mpya ya kuteka maji kisima cha Mkuyuni  kuwa ni siku tatu kwa wiki.
 Dhuluma Na Mateso
 Askari 11 anaeleza jinsi walijaribu kumgeuza mhutumiwa Fulani aache kuwa jiwe awe binadamu.Walimng’oa kucha za mkono na za miguu, walimgeuza kuwa popo na baadaye walifika katikati ya miguu yake na kupiga kambi hapo.badaye walimuua na kumzika msituni.uk 43
Mwelusi anafungwa gerezani kama hakuna kesi na hajahukumiwa.Batuanapomtemebela baada ya kumshawishi akiri kutochochea Wanabutangi na kushindwa anawaagiza Askari wazidi kumchapa na kumtesa.uk 29
Katika uk 30 Mwelusi anasema anachomwa na mikuki mia moja na anaelezwa kama anayeumia.Hii ni kutokana na kichapo anachopata kutoka kwa Askari.
Uk49 Andua anasema kuwa hakupigana alipigwa na ndia sababu ako na jeraha upande mmoja wa uso wake.Anasema kuwa ni Ni Askari waliwapiga kule kisima cha Mkuyuni baada ya wao kwenda kuteka maji.
Askari wa Butangi kulingana na Tanya si wa kulinda mbali ni wa kuleta mateso na kuwachapa Wana butnagi. Tanya anasema kuwa juzi walimngoa motto wa Chendeke meno.
Uk 24 Mweke na Talui wanapokuja kuzungumza na Mwelusi wanafanya hivyo kwa makofi na mateka.Mwelusi anasema kuwa taya zake zinawaka moto.
Batu anajaribu kuukinga uongozi wa Bokono na amamuomba mwelusi kuacha uchochezi na kuomba msamaha.Mwelusi anapokataa kukiri kwamba anatumiwa na majirani ili kuchafua Butangi. Anapotataa Batu anamwambia kuwa amepotoshwa . Batu anatoa ishara kwa Askari na kuondoka. Yeye anawpa ruhusa Askari wamtese mwelusi badala ya kumlinda.uk 36
Ubinafsi
Tunauona ubinafsi wa Gege .Uk wa 95 Gege anamuua Mwelusi nduguye ili apate kuozwa Alida bintiye Mtemi. Uk 17 anamuambia Mwelusi ajali maisha yake aachane na jamii. Gege hajali maisha ya wnabutangi wengine anajijali yeye mwenyewe.
Uk 89 Kaloo anamtuma zigu kwa Bokono amshukuru kwa ajili ya kazi aliyoamuru mototo wake apewe.kaloo pia hajali juu ya Butangi yeye anataka awe na uhusiano na Bokono ili apate mali zaidi.
Gege hajaenda kumtizama nduguye, Mwelusi kule gerezani.Gege anwambia mamayake asimzomee anapoulizwa.Anaendelea kutengeneza ala na kusema kuwa wasichana watamtambua .Hivyo anajali sana wasichana kuliko nduguye.uk43
Ukombozi
Mwelusi,Atega.Andua,Kame na Askari 1 ni baadhi ya wanamapinduzi katka Butangi.
Watu hawa wanapinga utawala wa Mtemi Bokono na vibaraka wake.
Wakati Mwelusi amefungwa gerezani Atega anamletea mkate wa wishwa ukiwa na tupa ambayo anatumia kukata minyororo na kujikomboa. Baadaye umati wa watu wanakuja na kumsaidia kufungua gereza na kujikomboa.uk 59
Kwa Uongozi wa Mwelusi wanaendelea kutetea haki zao.Mfano Andua anaenda kisimani kuteka maji.
Hata baada ya mwelusi kuuliwa na Gege wanamapinduzi hawa wanaendelea na harakati zao za ukombozi. Uk 105
Kitabu kinaisha kama Bokono,Batu,Zigu , Mweke na Gege wamefungwa kamba baada ya kufumaniwa na Waandamanaji.Hivyo wanaukombozi wanafaulu kukomboa Butangi kutokana na utawala Mbaya.
Mwelusi anadaiwa kuwa  yeye ndiye kiongozi wa kundi la kabakaba. Anahusika na shughuli za ukombozi.Ni yeye kiongozi wa kundi hili la wanamapinduzi.

 Usaliti
 Gege anamsaliti kakake, Mwelusi kwa Kumuua pale Kisimani. Uk 95 Gege anamdanganya Mwelusi kuwa ametumwa na mama yao Tanya huku akilia , ni ujumbe muhimu ambazo babayao alimwachia. Wanaenda chemba  na Gege anamuua.
Viongozi wa Butangi ikiwemo Batu na Zigu wanawasaliti kwa kuwanyima haki zao na kuwatesa.
Utu
Kame Askari 1 ni wenye utu wanamtetea Mwelusi.
Uk 60 wakati Batu na zigu wanataka kumuua Mwelusi Kama anasema wamuachiliea kwa kuwa hana makosa yoyote.
Uk 35 Tanya anapowaomba Askari kumwona mwanawe Askari 11 na 111 wanamkazata. Askari 1 anamuhurumia Tanya na kuwaomba wenzake wamkubalie mama huyo kumwona mwanawe.
Hawa wawili paoja na wengine kama vile Azena na Atega ni wenye utu miongoni mwa wanabutangi wengi ambao wana unyama kama vile Batu.
Askari wanapanga kula chakula cha mfungwa lakini Askari 1 anawakataza na kuwaomba wampe mfunwa chakula chake.uk 37
Unafiki
Uk 25 Mweke na Talui wanamhadithia Gege jinsi harusi yake na Alida itakavyokuwa. Wanamwambia Gege amuue Nduguye Mwelusi na atapewa mali pamoja na kuoa mtotot wa Mtemi Bokono.
Wakati Gege anaenda kudai malipo yake Baada ya kumuua Mwelusi ndio anagundua kuwa alidanganywa.Talui na Mweke ni wanafiki walijua kuwa wanamdanganya Gege ili awasidie tu kumumaliza Mwelusi.
Batu anapomtemebelea Mwelusi gerezani anamwambi a kuwa ni rafiki yake na kumuomba ajiunge naye katika kuitumikia Butnangi.Huu ni unafiki kwani kabla ya hapo alipokuwa kwenye mkutano na Zigu na Kame alpanga jinsi watakavyo muua.
Uk 79  Batu anapomtembelea Tanya anamwita rafiki yake tangu ujana wao.huuni unafiki kwani Batu yuko pale kumtafuta Mwelusi.
Baada ya kumuahidi Tanya kuwa watampa Mwelusi chakula Askari wanakula chakula hiki na Kumuomba askari 1 ampelekee rafiki yake mkate wa wishwa. Uk 58. Huu ni unafiki.

Uchochezi
  Kabla mkutano uanze Mwelusi anafika pale na kudai kuwa anapita.Hata hivyo nia yake wakiwa na Atega ni kuwachochea watu wasuhudhurie mkutano wa Mtemi Bokono.Uk 1
Uk wa 9 Zigu anasema kuwa kuna fununu ya kuwa kuna kijana anayechochea watu.Kijana huyu ni Mwelusi.
Uk 90 Zigu anamwambia Kaloo kwamba Bokono amekuwa akimtaja mara kwa mara.Zigu ananchochea Kaloo aonane na Bokono na kumpa shukrani yeye mwenye kwa kazi ambayo Bokono alamuru motto wa Kaloo apewe.

FALSAFA YA MWANDISHI
Mwandishi analenga kuzindua wananchi kuhusu utawala mbaya.Anatetea haki za walionyanyaswa na kukandamizwa. Anashikila kuwa kuna uwezo wa kujikomboa kutoka kwa uongozi mbaya .Hii ni kupitia kwa watu kuungana na kuandama na kutetea haki zao na kubadilisha uongozi mbaya ,pamoja na kuwafungaviongozi wabaya.
Falsafa ya Kithaka ni haki na hukumu kwa wenye makosa.
NADHARIA
Mwandishi ametumia Nadharia kama vile Umaksi.Katika Butangi wenye mali wananyanyasa wasio na mali.Kuna Ufeministi kwani Atega ,Andua Tanya na Azena ni wahusika wa kike wanaoshiriki katika ukombozi.Kuna Uhalisia Kwani matukio ni ya kawaida kam vile uongozi mbaya na kunyimwa haki katika maisha ya kila siku. Kuna Utamaushi kwani wanabutangi wamekata tama.MfanoTanya anamtaka Mwelusi aondoke Butangi
HITIMISHO
Mwandishi amefaulu kutumia mbinu na kutoa maudhui kwa kutumia nadharia. Kithaka anatetea haki kwa wenye Kunyanyaswa na hukumu kwa wenye makosa.Amewatumia wahusika wa kawaida kuutoa ujumbe wake.
Kuna udhaifu katika anwani kwani sio wahusika wote wanaathiriwa na kifo kisimani.Kitabu kimeshughulikia zaidi ya kifo.

UHUSIANO KATI YA TAMTHILIA YA KIFO KISIMANI NA UTENZI W A FUMO LIYONGO
Utenzi wa fumo liyongo unamhusu shujaa Liyongo kutoka jamii ya waswahili.liyongo alishuhudiwa na jamii yake na makabila jirani kama vile wagalla.

Hata hivyo mfalme wa pate(Daudi Mringwari) alimchukia kwa kuhofu kuwa angemnyang’anya  utawa wake.Hivyo alipanga njama za kumwangamiza liyong.Akamtia gerezani alikolindwa na Askari wake.Akiwa gerezani, aliletewa mkate wa wishwa uliotiwa tupa.Aliitumia tupa hii kukata minyororo kasha akotoroka.

Mfalme wa pate hakukata tama.Alimshawishi mwanawe Liyongo kumuua babake na kumwahidi kumwoza bintiye.Liyongo akauliwa na mwanawe kwa kumfuma msumari wa shaba kitovuni.Liyongo alifia kisimani na kuwatisha watu wasichote maji kwa siku kadhaa.

Utenzi huu kwa kiasi kikubwa unahusiana na tamthilia ya Kifo Kisimani, inayomhusu Mwelusi anayepinga utawala dhalimu wa Mtemi Bokono. Anachukiwa na Bokono pamoja na vibaraka wake kwa hofu kuwa atauangusha utawala huo.Anatiwa gerezani lakini anatoroka baada ya kukata minyororo kwa tupa iliyotiwa ndani ya mkate wa wishwa alioletewa na Atega. Bokono anamtumia nduguye Mwelusi,  Gege kumuua kwa kumdunga kisu pale kisimani. Gege vilevile anaahidiwa na Mweke wakiwa na Talui kuwa ataozwa bintiye mtemi.Alida.

Hata hivyo kuna tofauti nyingi kati ya tungo hizi mbili. Fumo Liyongo ni mhusika wa kihistoria, aliishi baina ya karne 15 na 16.Mwelusi naye ni mhusika wa kubuni.Fumo alikuwa na sifa za kiajabu kama vile nguvu zilizokithiri, mpiganaji hodari aliyeshinda vita vingi, ukubwa uliopita kiasi na uwezo wa kutambua mabo kabla hayajiri.Mwelusi hana sifa kaa hizi zinazomtambuliasha kama mhusika wa kipekee.Vita anavyopigana si vya silaha bali anapinga dhuluma na mateso kwa Wanabutangi.

MAREJELEO.
  1. Kithaka wa Mberia, (2001) Kifo Kisimani, Marimba Publications limited, Nairobi Kenya.
  2. Rocha M.Chimera, (1998) Kiswahili; Past, Present and Future Horizons,Nairobi University Press,.Nairobi.


Visit our website and leave your comment : https://freekcserevisionpapers.blogspot.com
ALSO OTHER BOOKS AVAILABLE
1. mwongozo wa Mwenda wazimu by Mbatiah
2. mwongozo wa Siku Njema by ken walibora
3. mwongozo kifo kisimani
+more dOWNLOAD APP FOR FREE'BRILLIANT LEARNERS'……………………………………………………………………………………………….

GET LEANRNING RESOURCES FOR FREE. DOWNLOAD 'BRILLIANT LEARNERS' APP FOR FREE ON PLAYSTORE OR USE THESE LINK. https://play.google.co...